Vanessa Mdee ameachiwa kwa dhamana jana jioni

0
229

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee A.K.A Vee Money ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kushikiliwa kwa siku nne kufuatia tuhuma ya dawa za kulevya inayomkabili.

Mdee aliachiwa jana jioni ambapo anatuhumiwa kutumia na kusambaza dawa za kulevya.

Alishikiliwa na Polisi tangu wiki iliyopita baada ya kwenda kuripoti kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa hizo.

Vanessa alishikiliwa muda mfupi baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini alipokwenda kwa ajili ya kazi zake za kimuziki.

Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva waliotajwa na na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

 

LEAVE A REPLY