Vanessa Mdee amaliza bifu na Mimi Mars

0
199

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amemaliza bifu iliyokuwepo kati yake na mwanamuziki mwenzake Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wake.

Vanessa amesema kuwa kuwa kwa sasa hana tena bifu na msanii huyo ambaye ni mdogo wake huyo kwa kuwa bifu hazina maana yoyote.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kuwa ameamua kumaliza tofauti kati yake na ndugu yake huyo kwa kuwa wao ni ndugu hivyo hakuna maana yoyote wao kutofautiana kwa aina yoyote ile katika maisha yao.

Amesema kuwa “Naona ni jambo jema kwa kuwa mimi na mdogo wangu tulikuwa hatupo pamoja kutokana na sababu tu ambazo hazina msingi.

Pia Vanessa ameongeza kwa kusema kuwa Kwa hiyo nimeona tumalize bifu letu na tuendelee kupeana sapoti katika kazi zetu japokuwa kila mmoja anafanya muziki wake.

Mwanamuziki huyo ambaye kwasasa anamiliki lebo ya muziki ijulikanayo kama Mdee Music ambapo pia mdogo wake huyo yupo chini ya lebo hiyo.

LEAVE A REPLY