Vanessa Mdee achora tattoo ya jina la mpenzi wake

0
49

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ameamua kuchora tattoo ya jina la mpenzi wake Rotimi ambaye ni muigizaji wa filamu ya Power nchini Marekani.

Vanessa ameonesha tattoo hiyo iliyochorwa sehemu ya kifuani kwake, kwenye picha yake mpya ya pamoja akiwa na mpenzi wake huyo raia wa Marekani.

Hata hivyo kwa wawili hawa walioko penzini ambao hufanya ishara za kufanana katika kuashiria upendo kati yao, bado haijabainika kama Rotimi naye kachora tattoo ya jina la Vanessa Mdee kwenye mwili wake.

Wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi ambapo hivi karibuni walivarishana pete ya uchumba wakiashiria ndoa ya wawili hao ipo karibuni.

Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwasasa anaishai nchini Marekani na mpenzi wake huyo baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux.

LEAVE A REPLY