Vanessa akanusha kuachana na Jux

0
221

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka na kusema kukanusha kuachana na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja baada ya kuenea habari katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao kwasasa hawapo pamoja jambo ambalo mwanamuziki huyo amelipinga vikali.

Habari zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilisema kuwa sababu ya kuachana kwao ni kwasababu Jux alimsaliti Vanessa kwa mwanamke mwingine.

Vanessa amesema hana tatizo kabisa na Jux ila kazi ndiyo zinazowafanya wasiwe karibu hivyo watu kuona kama hawapo sawa.

“Mimi na Jux hatuwezi kuwa pamoja kila siku kuna kipindi kazi zinabana sana na ndio maana watu wanaona tumemwagana, niwatoe hofu tu mashabiki zangu kwamba tupo sawa na hakuna kitu chochote kibaya kinachoendelea kati yetu zaidi ya ubize wa kazi unaotufanya tuwe mbali,” alisema Vaness

LEAVE A REPLY