Vampire Diaries kuishia ‘Season 8’

0
274
Mashabiki na wapenzi wa ‘series’ kali ya ‘The Vampire Diaries’ wanapaswa kutafuta shughuli nyingine ya kufanya ili kuutumia muda wao vizuri.
Ukweli wa mambo ndio ambao umelazimisha jambo hilo baada ya waandaaji wa tamthiliya hiyo kutangaza kuwa ‘mzigo’ utaishia kwenye msimu wa 8.
Vampire Diaries ambayo imeshaonyeshwa kwa misimu 7 nchini Marekani ni moja ya series ambazo zimevutia mashabiki wengi wa filamu nchini Tanzania na Afrika Mashariki.
Maprodyuza wakuu wa tamthiliya hiyo, Julie Plec na Kevin Williamson wametangaza kuisha kwa tamthiliya hiyo kupitia Comic-Con ambalo ni kongamano la mwaka la wataalamu wa tamthiliya.
Miongoni mwa mastaa wa Hollywood waliocheza filamu hiyo ni Paul Wesley na Ian Somerhalder.
Msimu wa mwisho wa Vampire Diaries utakuwa na sehemu (episodes) 16 na utazinduliwa tarehe 21 Oktoba.

LEAVE A REPLY