Uwoya awachana wanaofuatilia maisha yake

0
154

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amewajia baadhi ya watu waliokuwa wakizusha baadhi ya maneno kuhusu mahusiano yake ya sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram muigizaji huyo amewataka watu hao kuacha kufuatilia maisha yake badala yake wafanye maisha yao.

Ameandika “mhhhh bongo jamani, mara natembea na john mara na musa , mara uritho mara mafao ya baba yake, mara hana lolote kwakweli kazi mnayo  na ndio maana hamna kazi za kufanya jua likisogea na nyie mnasogea.daaah ..poleni sana kifupi tu ni kwamba mnajisumbua sana fanyeni maisha yenu”

Kauli ya Uwoya imekuja baada ya tetesi zikidai kuwa muigizaji huyo kwa sasa yuko katika mahusiano na kigogo mmoja anaefanya kazi katika serikali ya kenya.

Maneno ya mashabiki yamekuwa mengi kutokana na kuwa muigizaji huyo amekuwa akioneana akila bata maeneo mbalimbali ikiwemo nchini Dubai pamoja na kufanya sherehe tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Pia Uwoya amesema kuwa watu wamekuwa wakiangaika sana kufatilia maisha yake na kusema mara anatoka na huyu mara yule lakini hakuna mwenye ukweli zaidi ya yeye mwenyewe hivyo waache kumfatilia.

 

LEAVE A REPLY