Uwoya amwagia sifa Alikiba

0
129

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amesema kuwa anamkubali mwanamuziki AliKiba huku akitaja Wimbo wa Hadithi kuwa ndiyo wimbo wake pendwa wa muda wote.

 

Uwoya amefunguka hayo baada ya kuhudhuria kwenye tamasha la msanii huyo la kufunga mwaka lililofanyika Club Next Door Arena iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam Desemba 29 mwaka huu.

 

Muigizaji huyo mwenye mvuto wa aina yake Bongo amesema kuwa hajawahi kuonekana akiwa karibu na Kiba lakini ni mtu anayeikubali kazi yake.

 

Uwoya pia amezungumzia kuhusiana na suala la kuzindua club  yake aliyotarajiwa kuizindua usiku wa tarehe 23, lakini amesema kuwa hakufanya hivyo kwa kuwa kuna vitu havikukamilika kwa wakati.

 

Alikiba alifanya sherehe yake ya kufunga mwaka katika ukuimbi wa Next Door Arena ambapo alikuwa na wanamuziki wenzake kama vile Mwana FA, Nuh Mziwanda, Barababa na wengineo.

LEAVE A REPLY