Uwoya adai hana bifu na Dogo Janja

0
101

Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa hana tatizo na aliyekuwa mume wake mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja licha kuachana.

Irene Uwoya na Dogo Janja waliweka wazi kuwa wameachana siku chache zilizopita baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miezi kadhaa.

Baada ya kuingia kwenye mvutano mkali iliyopita na hata kurushiana madongo kwenye Mitandao ya kijamii hatimaye Uwoya amesema hana Bifu na Dogo Janja.

Uwoya ameweka wazi kuwa ndoa yake na Dogo Janja imevunjika lakini sio kitu cha ajabu kwani ndoa nyingi zimeshawahi kuvunjika katika siku za nyuma.

Wawili hao wameachana na kila mmoja ameanzisha mahusiano yake mengine baada ya ndoa yao kuvunjika ramsi mwisho wa mwaka jana.

LEAVE A REPLY