Uturuki yawashikilia majenerali 85 kwa kuhusika na njama za mapinduzi nchini humo

0
123

Zaidi ya majenerali 85 na maamiri wa jeshi nchini Uturuki wapo ndani wakisubiri hukumu yao kuhusiana na mpango wao wa mapinduzi ulioshindikana nchini humo wiki iliyopita.

Waliokamatwa ni pamoja na mkuu wa zamani wa vikosi vya wanaanga jenerali Akin Ozturk anayetuhumiwa kuandaa njama hiyo na jenerali Adem Hududi anayeongoza kikosi cha pili cha jeshi la Uturuki chenye jukumu la kukabiliana na vitisho kutoka nchi za Syria, Iran na Iraq.

Viongozi wa Uturuki wamewakamata maelfu ya wanajeshi na wanasheria kwa dhana za kushiriki katika njama iliyoshindwa ya mapinduzi Julai 15 ambapo watu 232 wamepoteza maisha yao.

Serikali ya Uturuki inamtuhumu,Shekh Fetthulah Gulen anayeishi nchini Marekani kwa kuhusika na njama ya kutaka kuipindua serikali ya rais, Reccep Tayyip Erdogan.

LEAVE A REPLY