Utawala wa Trump kukata rufaa baada ya mahakama kuzuia pingamizi la waislamu kutoingia Marekani

0
272

Utawala wa Trump umewasilisha rufaa ya kutaka kurejeshwa kwa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia wa mataifa saba ya waislamu kusafiri hadi Marekani baada ya mahakama kuipinga amri hiyo.

Tangazo hilo linafuatia misururu kadhaa ya tweeter kutoka kwa Trump ambapo anampinga jaji aliyetoa uamuzi huo, huku akionya kuwa watu wabaya na hatari, huenda wakamiminika hadi Marekani kutokana na uamuzi huo.

Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege, yangali bado yanawakubalia raia kutoka mataifa hayo husika, kuabiri ndege na kuingia Marekani.

Kumekuwepo na maandamano dhidi ya marufuku hiyo ya Trump huko Washington, jimbo la Miami na miji mingine kadhaa ya Marekani, pamoja na miji mingine mikuu ya bara Ulaya.

LEAVE A REPLY