Utani wa Baba Levo kwa Peter Msechu

0
130

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amesema huwa anamshambulia kwa maneno Peter Msechu kwa sababu anataka apungue hadi awe na mwili kama wa Vanessa Mdee.

Baba Levo amesema huwa anajisikia raha pale anapomshambulia Peter Msechu na lengo lake ni kumtaka akonde na kumpa mawazo.

“Najisikia raha ninapomshambulia Peter Msechu, lengo la kumshambulia huwa nataka akonde na nimpe mawazo ili awe na mwili flani hivi kama Vanessa Mdee.

 Baba Levo amesema kuwa nataka hata akitembea awe sawa na Vanessa, ila siwezi nikamtania hadi kumvunjia mipaka yake kwa mfano kufika hadi kwa wazazi”.

Wawili hao wamekuwa na utani wa siku nyingi hivyo utani wao huo unakuwa kama kiburudisho kwa mashabiki wao wa muziki.

LEAVE A REPLY