Utafutaji wa maisha Ulaya: Kipa wa timu ya taifa ya wanawake ya Gambia afia baharini

0
336

Timu ya taifa ya wanawake ya Gambia imekumbwa na mstuko mkubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa golikipa wa timu hiyo Fatim Jawara.

Fatim Jawara aliyefariki kwa kuzama baharini wakati akijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean ili kwenda Ulaya alikuwa na miaka 19.

Rais wa chama cha soka cha nchi hiyo, Lamin Kaba Bajo pamoja na familia yake wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Fatim alikumbwa na mauti hayo baada ya boti aliyopanda kutoka Libya kupinduka baharini na baadhi ya abiria akiwemo yeye kupoteza maisha.

MUNGU AMSAMEHE MAKOSA YAKE NA AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI: Amin

LEAVE A REPLY