Utafiti: Warefu zaidi na wafupi mno duniani wajulikana

0
340
Utafiti uliofanywa na kuchapishwa kwenye jarida eLife umegundua kuwa wanaume wa Uholanzi na wanawake wa Latvia ndio wanaoongoza kwa urefu zaidi duniani.
Wastani wa mwanaume wa kiholanzi ni 183cm (6ft) tall, wakati wastani wa mwanamke wa Latvia ni 170cm (5ft 7in).
Utafiti huo ulikuwa unafuatilia mwenendo wa ukuaji kwa nchi 187 kuanzia mwaka 1914.
Utafiti huo pia umegundua kuwa wanaume wa Iran na wanawake wa Korea Kusini wameongezeka urefu kwa haraka sana kwa wastani wa 16cm (6in) and 20cm (8in).
Wanaume wanaotokea Timor Mashariki ndio waliogundulika kuwa wafupi zaidi duniani wakiwa na wastani wa urefu wa 160cm; 5ft 3in.
Wanawake wa Guatemala ndio wafupi zaidi duniani huku wakiendelea kushikilia nafasi hiyo tangu mwaka 1914.
Kwa mujibu wa utafiti huo, wanawake hao karne moja iliyopita mwanamke mwenye miaka 18 kutoka nchi hiyo alikuwa na wastani wa 140cm (4ft 7in) na hadi utafiti huo unachapishwa walikuwa hawajafika 150cm (4ft 11in).

LEAVE A REPLY