Utafiti mkubwa wa chanjo ya VVU/UKIMWI kufanyika Afrika Kusini mwaka huu

0
332

Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa VVU/UKIMWI cha Desmond Tutu HIV Centre na rais mteule wa jamii ya kimataifa ya International AIDS Society, Linda Gail Bekker amesema kuwa majaribio mapya ya chanjo ya ukimwi yatafanyika tena nchini Afrika kusini baadae mwaka huu.

Kituo hicho kinaogoza utafiti wa awamu ya pili wa chanjo ya VVU/UKIMWI na tayari majaribio madogo yanayojulikana kwa jina la HVTN100 yalifanyika Afrika Kusini mwaka jana kujaribu kiwango cha usalama na nguvu ya kinga ya mwili ambayo chanjo hiyo inaweza kuupa mwili wa binadamu huku mkakati ukiwa ni kufanya majaribio kwenye sehemu kubwa ya waathirika wa ugonjwa.

Kwenye utafiti wa mwaka 2015 watu 252 walijitolea kupewa chanjo hiyo mpya ijulikanayo kwa jina la ALVAC-HIV/gp120 au kupewa plasebo ili kupima kiasi cha kinga kitakachozalishwa.

Mwaka 2015 maambukizi mapya 2.1m yaliripotiwa kutokea duniani ambapo robo tatu yalitokea Afrika.

VVU/UKIMWI: Watafiti wakiwa kazini
VVU/UKIMWI: Watafiti wakiwa casino

LEAVE A REPLY