Ushauri wa Sister Fey kwa Kajala

0
58

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Faidha Omary ‘Sister Fey’ amefunguka kuwa msanii wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja anatakiwa kuwa makini na Harmonize kwa upande mwanaye Paula.

Sister Fey amesema kuwa Kajala anatakiwa kuwa makini sana na Harmonize kwa sababu wanaume wanabadilika muda wowote hivyo asiwe anamuachia sana wawe karibu.

“Kajala asiwe anamuachia sana Paula kuwa na Harmo ni hatari, unajua Harmonize bado damu inachemka, awe makini,” alisema Sister Fey.

Sister Fey amesema kuwa siyo kama anaona wivu mapenzi ya wawili hao ila anatoa ushauri kwa mwanamke mwenzake kwasababu Harmonize bado kijana na damu inachemka.

LEAVE A REPLY