Ushauri wa Ray kwa wanawake wanaonyonyesha

0
218

Muigizaji wa Bongo Movie, Vicent Kigosi maarufu kwa jina la Ray amewapa somo wanawake wasiopenda kunyonyesha watoto.

Kupitia akaunti yake Instagram ameandika ‘Unamkuta mdada kajifungua mtoto eti anaogopa kumnyonyesha mtoto wake kwa kipindi kirefu akiogopa  maziwa yake kuanguka bila kujua kama maziwa ya mama ni lishe bora ya mtoto kuliko vyakula vyote unavyovijua wewe.

Pia ameongeza kwa kuandika “Kumfanya mtoto kutoumwa mara kwa mara kumfanya mtoto awe mchangamfu muda wote coz maziwa ya mama ni kinga kubwa sana kwa mtoto kitaalamu hata kidini kama sijakosea wanakwambia mtoto lazima anyonye kwa muda wa miaka miwili, sasa je hao madada kwa kipini hiki wapo?.

Maana unamkuta madada kajifungua mtoto leo baada ya wiki utamkuta yupo disco anaruka majoka sasa hapo unategemea mtoto awe na afya gani ndio maana hata kwa madada wanaofanya kazi kipindi wajifunguapo utapata miezi mitatu ya kupumzika angalu basi mtoto apate malezi bora ya mama kitaalam wanaita (maternity leave) kama umeamua kuwa na mtoto jitahidi kumpa malezi yanayostahili kama mzazi.

Kwa kweli nimpongeze sana Chuchu kwani ni mwanamke wa tofauti sana maana mpaka sasa bado mtoto wetu ananyonya maziwa yake bila kuogopa wale kujali kama yataanguka na kizuri zaidi kaniambia mpaka ifike miaka miwili ndio mtoto atamuachisha kumnyonyesha.

Ray amesema hayo baada ya kupokea ujumbe mwingi kutoka kwa watu mbali mbali zikimtaka kueleza siri ya mtoto wake na Chuchu Hansy, Jaden kukua haraka.

LEAVE A REPLY