Ushauri wa Mo Music kwa Dogo Janja kuhusu Irene Uwoja

0
88

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Mo Music ameibuka na kumpa ushauri Dogo Janja na kumtaka kuachana na mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya ili aepukane na matatizo.

Mo Music amesema kuwa yeye anapenda kumshauri mwanamuziki huyo aachane na Irene Uwoya kwani siyo saizi yake katika mahusiano ya kimapenzi kwakuwa muigizaji huyo ana jina kubwa kuliko Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni ndoa hiyo ilisemekana kusambaratika baada ya Irene Uwoya kuonekana na wanaume wengine katika mitandao ya kijamii nchini Dubai jambo ambalo limeibua hisia za watu kuwa uhenda wawili hao ndoa yao ipo mashakani.

Pia Dogo Janja ameonekana kama mtu mwenye msongo wa mawazo kiasi ya kwamba kuonekana kwa Mwanasaiokolojia siku chache zilizopita.

Mo Music ameibuka na kumshauri msanii mwenzake kuachana na Uwoya kwani asipofabya hivyo anamtabiria kukutana na Kifo mbeleni kutokana na msongo wa mawazo.

LEAVE A REPLY