Ushauri wa Kiba kwa mastaa wa kike Bongo

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amewataka wanawake maarufu kwenye soko la muziki na filamu Tanzania kuitumia ipasavyo mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Alikiba anayetamba na ngoma ya ‘Mvumo wa Radi’, aliyasema hayo juzi alipohojiwa na kituo kimoja cha runinga jijini Dar es Salaam.

Ally Kiba, aliwatolea povu mastaa wa Bongo akiwataka waache  maisha ya kuigiza na kujianika uchi mitandaoni.

“Stara ni kitu kizuri sana katika jamii na maisha yetu kwa ujumla, mastaa wengi hasa dada zetu wanaamini kukaa utupu ndio kupendwa, lakini sisi wanaume hatuko hivyo,”.

LEAVE A REPLY