Ushauri wa AT kwa Babu na Papii Kocha

0
141

Mwanamuziki wa Mduara nchini, AT ametoa ushauri mzito kwa Babu Seya na mwanawe Papii Kocha kuwa mbali na baadhi ya watu huku akiwtahadharisha kuhusu kiki.

AT amemtaka Babu Seya awe makini sana na watu wanaomzunguka wanapomshauri juu ya Kiki na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Mwanamuziki huyo ambaye kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Kazi’ AT amesema kuna watu wengi ambao watakuwa hawapendi kumuona Babu Seya na mwanae wakifanikiwa katika maisha yao mapya baada ya kutoka jela.

Pia AT amesema kwamba yeye alipata shida sana haswa pale alipoanza kusikiliza maneno na ushauri wa mashabiki hali iliyopelekea mpaka akabadilisha aina ya mziki ambao alikuwa anaufanya na kuhamia katika Bongo fleva kitu ambacho anaamini kwamba kilimrudisha nyuma kisanaa.

Kwa upande wa mziki wake AT amesema ameamua kujikita rasmi katika mziki wa mduara mpaka ahakikishe anarudisha heshima ya jina lake ambalo anaona linapotea na kipindi hiki hatosikiliza ushauri wa mtu yeyote ambaye atamshauri kinyume na mipango yake.

LEAVE A REPLY