Usain Bolt arejea uwanjani kwa ushindi wa mita 200

0
105

Mkimbiaji mahiri wa Jamaica ambaye alikuwa shakani kushiriki mashindano ya Olimpiki baadae mwaka huu nchini Brazil, Usain Bolt amethibitisha kuwa yuko tayari kushindana baada ya kushinda mbio za wanaume za 200m kwenye michezo ya kumbukum,bu kwenye uwanja wa Olimpiki wa jijini London.

Bolt alitumia sekunde 19.89 kumaliza mbio hizo ambapo alitofautiana na Alonso Edward aliyeshika nafasi ya pili kwa sekunde 0.15.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mshindi wa medali ya shaba ya michezo ya Jumuiya ya Madola kutoka Uingereza, Adam Gemili aliyekimbia kwa sekunde 20.07.

Ushindi huo wa Bolt unaonekana kushusha presha ya timu yake ya taifa baada ya kushindwa kuhudhuria mbio za mchujo mapema mwezi huu kutokana na majeraha ya mguu.

Mpaka sasa Bolt ndiye mshindi wa medali za dhahabu za Olimpiki kwa mbio za mita 100 na mita 200 zilizofanyika London na Beijing na atatetea mataji yake nchini Brazil.

Mpaka sasa Bolt ndiye anayeshikilia rekodi ya kukimbia kwa kasi zaidi zaidi duniani, rekodi ambayo aliiweka mwaka 2009 kwa kukimbia kwa umbali wa mita 200 kwa sekunde 19.19

LEAVE A REPLY