Urusi yafungiwa kushiriki Olimpiki 2016

0
140

Mahakama ya upatanishi michezoni (CAS) imekataa rufaa ya kamati ya olimpiki ya nchi ya Urusi pamoja na wanamichezo 68 wa nchi hiyo ya kushiriki kwenye michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil baadae mwaka huu.

Wachezaji wa Urusi wamefungiwa na Shirikisho la kimataifa la IAAF na CAS imeunga mkono hukumu hiyo iliyotolewa tangu Novemba mwaka 2015.

Adhabu ya kufungiwa huko ilikuja kufuatia ripoti ya shirika linaloshughulikia uzuiaji wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni (WADA) kuonyesha kuwa wachezaji wa Urusi walikuwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu.

Mapema wiki hii WADA na mashirika mengine yaliiomba kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) na kamati ya kimataifa ya wachezaji walemavu kuifungia Urusi kushiriki mashindano ya Rio de Janeiro (2016) na IOC ilikubali na kutoa tangazo la kuifungia Urusi.

Nchi ya Urusi imeendelea kupinga vikali adhabu hiyo na kudai kuwa haki za kimsingi kabisa za michezo zimekiukwa na taasisi hizo.

LEAVE A REPLY