Upepo mkali kuvuma mikoa ya Dar, Mtwara na Pwani, wananchi watakiwa kuchukua tahadhari

0
246

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya Pwani ya Tanzania.

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka hiyo kupitia taarifa yao imesema kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2.

Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania.

Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

Hali hiyo ya hewa hiyo inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei mwaka huu kulingana na taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY