Upelelezi wa kesi ya Malima wakamilika

0
161

Upelelezi dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima umekamilika.

Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa kutajwa.

Hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru.

Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.

Katika hati ya mashtaka ilidaiwa kuwa, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

Ilidaiwa kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala alishindwa kuwasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake kwa kuwa Hakimu husika anaudhuru.

Mapema mwezi huu, Kibatala aliitaarifu Mahakama kuwa jana  angewasilisha pingamizi kuwa shtaka linalomkabili Malima, maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.

LEAVE A REPLY