Uongozi wa Ommy Dimpoz wawatoa wasi wasi mashabiki wa msanii huyo

0
142

Uongozi wa Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz umekanusha vikali taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa mwanamuziki huyo amefariki dunia nchini Ujerumani anapopatiwa matibabu.

Uongozi huo umesema hayo baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa msanii huyo alikuwa katika hali mbaya na kapatwa na umaauti kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Uongozi huo unasema kuwa taarifa hizo sio za kweli kwa sababu msanii wao mpaka sasa anaendelea  poa na kwamba hali yake inazidi kuimraika na kubadilika siku hadi siku sio kama ile aliyokuwa nayo hapo awali.

Msanii huyo ambae aliwahi kuripotiwa zaidi ya mara moja kuwa mgonjwa sana, amekuwa akirudihswa hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuangaliwa hali yake ingawa kuna kipindi aliwahi kuonekana kuwa imara zaidi kutokana na kuanza kuonekana katika mitandao ya kijamii.

Uongzio huo umewatoa wasiwasi mashabiki wa msanii huyo huku ukiwataka kuwa na maombi kwa ajuli ya msanii wao ili aweze kutoka katika majaribu hayo.

LEAVE A REPLY