United 2 Hull City 0: Mourinho akaribia ubingwa wa kwanza akiwa United

0
181
Manchester United's P

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amezidi kusogea karibu na ubingwa mkubwa akiwa na timu hiyo baada ya kikosi chake kushinda 2-0 dhidi ya Hull City.

United waliokuwa nyumbani Old Trafford ilikuwa ikipambana na Hull City kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi maarufu kama EFL.

Mourane Fellaini na Juan Mata ndio waliohakikisha United inajiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kupitia mabao yao ya kipindi cha pili.

Timu hizo zitarudiana Jaanuari 26 na mshindi atakutana na aidha Liverpool au Southapton ambazo zitapambana leo usiku kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya pili.

Hata hivyo Mourinho amechukizwa na kitendo cha wachezaji wake kushangilia kwa muda mrefu bao lililofungwa na Juan Mata.

LEAVE A REPLY