‘Unga’ ni vita ya zaidi ya jamii na mastaa wa Bongo Fleva…..cheki

0
683

Unajua kuwa madhara ya dawa za kulevya hayako tu kwa mastaa wa Bongo Fleva au mastaa wa Bongo Movie?

Unajua kuwa ingawa ni siri kubwa baina ya waathirika wa dawa za kulevya familia zao lakini bado kuna watu wako tayari siku zote kuwasaidia wengine kwa kutoa siri za ndani?

Hemed PhD ametuambia siri hiyo…….Hemed PhD ameweka wazi kuwa yeye ni mmoja wa wahanga wa utumiaji wa dawa za kulevya ambapo baba yake mzazi alikuwa mmoja wa waathirika wa dawa hizo na hiyo ikamuathiri kisaikolojia.

Athari ya wazazi kuwa waathirika wa dawa za kulevya pia iliwakumba watoto wa staa wa Bongo Fleva, Q-Chillah.

Lakini pamoja na Hemed kumuuguza mzazi wake ambaye alikuwa teja, yeye hakufikia kutumia dawa hizo.

Je, nawe una waathirika nyumbani kwenu ambao wanaweza kusaidia wengine wasiathirike?

Na, je ni watu wangapi ambao wameingia kwenye unga kutokana na ushawishi wa watu wao wa karibu?

LEAVE A REPLY