UNGA: Kauli 4 za kuhusika kwa Juma Nature na TID kwenye ulevi wa KR

0
936

Ni watu wachache sana miongoni mwa wapenzi wa sanaa ya Bongo Fleva ambao hawajui mkasa uliomkuta msanii KR Mullah a.k.a Jibaba CD 700 wikiendi iliyopita. Lakini kwa kifupi ni kuwa, KR alikutwa amelala (hajitambui) kwenye maeneo ya Temeke Mwembeyanga kwa kile kinachodaiwa kuzidiwa na kilevi.

KR ambaye ni memba wa zamani wa kundi la TMK Wanaume kwa sasa ni rais wa lebo ya Radar Entertainment iliyokuwa inaongozwa na mwanzilishi wake Khaleed Mohamed a.k.a TID.

Kabla ya kuondoka kundi la TMK na kujiunga na Radar Entertainment, KR alitahadharishwa juu ya jambo moja, ‘unga’!!

Sasa tujikumbushe juu ya kauli tata zinazohusiana na tukio la juzi:

Staa wa kundi la TMK Wanaume (kabla haijasambaratika) na mshkaji wa karibu wa KR, Juma Nature Kiroboto a.k.a Sir Nature alimtahadharisha KR kuwa, tetesi zilizopo mtaani ni kuwa TID anatumia dawa za kulevya (licha ya TID a.k.a Mnyama kukanusha mara kadhaa kutumia dawa hizo) hivyo asije kuiga maisha ya huko.

Kauli ya Nature kuhusu KR kuhamia Radar:

 Najua kuwa KR anatafuta maisha ya muziki na hivyo mimi sikatai yeye kuhamia kule lakini ajiangalie, awe makini asije akaharibiwa na maisha ya kule. Asiige mambo ya wale jamaa. Mambo ya kutumia madude yao yale’.

Kauli ya KR kuhusu kuhamia Radar na ushauri wa Nature: 

Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda nature anavyoona nipo huku (Radar Entertainment anaona kazi zake zitakuwa zinalega lega. Labda hajapendezwa mimi kufanya kazi na yule mtu (TID) na yeye alitegemea mimi nifanye nae kazi yeye tu. Aniache nitingishe’

Kauli KR Kuhusu TID kuvuta Unga

Kusema kweli zamani muda uliopita nilikuwa nasikia sikia taarifa lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu. Na kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akitumia au akifanya hayo mambo’.

TID aliwahi kudai kuwa Sir Nature ni msanii mchafu lakini Nature nae akajibu mapigo kwa kudai kuwa TID hawezi kumsaidia KR kutoka kimaisha kwasababu yeye mwenyewe bado anaishi kwa wazazi wake (analelewa).

Kauli ya Nature kuhusu TID kumtoa KR kimuziki

Yeye mwenyewe anaishi na mama yake na baba yake sasa atamtoaje mtu?

Baada ya tukio la juzi, Nature alianza upya kumlaumu TID ambaye hata hivyo hajajibu kitu na badala yake aliziondoa picha zake kwenye ukurasa wake wa INSTAGRAM bila kueleza sababu yoyote.

Kauli ya KR baada ya kukutwa ‘kazimika’

‘Ile ni hali ya kawaida tu, mitungi ilinizidia. Mbona mambo yale yanatokea sana tu. Mimi situmii dawa za kulevya’.

Kauli ya Nature baada ya KR ‘kuzima’.

‘Mimi nilishamwambia kule anakokwenda sio kuzuri, matokeo yake ndio haya sasa. Unadhani zile ni stimu za nini? Sio stimu za mitungi zile, mbona stimu za mitungi zinaeleweka wazi. Mi namlaumu sana TID kwa kutuharibia mtu. Ila KR ajijue tu kuwa anakoenda kubaya’

LEAVE A REPLY