UN yasubiri tamko la Burundi kuhusu kupeleka askari wake Bujumbura

0
125

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limeridhia kupeleka askari wake ili kusaidia kutuliza ghasia na kudhibiti vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Baraza hilo limeunga mkono pendekezo lililoandaliwa na nchi ya Ufaransa la kutuma askari 228 kwa kipindi cha kuanzia cha mwaka mmoja.

Hata hivyo Serikali ya Burundi haijatoa tamko rasmi la kukubali azimio hilo ingawa taarifa za awali zinasema Burundi iko tayari kupokea askari wasiozidi 50 wa UN.

Mpaka sasa zaidi ya watu 400 wamepoteza maisha nchini humo tangu vurugu zitokee baada ya rais Pierre Nkurunziza atangaze kuwania muhula wa tatu mwezi April.

Rais Nkurunziza alitangaza uamuzi wa kuwania awamu ya tatu ya madaraka ya urais baada ya kumalizika kwa kipindi cha muhula wa pili wa uongozi wake uamuzi ambao unaenda kinyume na katiba ya nchi hiyo inayotaka madaraka ya rais yaishie kwenye mihula miwili tu.

LEAVE A REPLY