UN yaonya kuhusu uhaba wa fedha za kupambana na Boko Haram

0
163
(FILES) File photo taken September 17, 2008 shows fighters of the Movement for the Emancipation of Niger Delta (MEND) as they prepare for an operation against the Nigerian army in Niger Delta on September 17, 2008. MEND said January 30, 2009 that it was calling off the ceasefire it declared four months ago, following an attack by the army. AFP PHOTO / FILES /PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images)

Umoja wa Mataifa (UN) umetahadharisha kuwa mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram unakabiliwa na ukosefu wa fedha.

Mratibu wa masuala ya binadamu wa Umoja wa Mataifa, Stephen O’Brien amedai kuwa matendo ya Boko Haram yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao na idadi isiyojulikana kuwa kwenye uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu.

Umoja wa mataifa umelituhumu kundi hilo kufanya vurugu na ukatili mkubwa ‘usiofikirika’ nchini Nigeria.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 9 wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na matendo ya Boko Haram yaliyosambaa kutoka Nigeria na kuingia kwenye nchi nyingine za Afrika Magharibi.

Boko Haram iliwahi kutangaza kuwa ina ushirika na kundi jengine la kigaidi la IS.

Stephen O’Brien ameongeza kuwa ‘unyama, ukatili na matendo yasiyotumia akili yamepelekea uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kwenye nchi ya Nigeria’

‘Tangu Januari hadi Juni 2016 zaidi ya watoto 50 wamelazimishwa kubeba mabomu ya kujitoa mhanga kwenye nchi nne za Afrika Magharibi’

Mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa (UN) Jeffrey Feltman amesema kuwa Boko Harm imeendelea kuwa tishio kwa ustawi wa usalama wa kanda hiyo licha ya kuondolewa kwenye baadhi ya maeneo.

Wawakilishi hao wa Umoja wa Mataifa, Stephen O’Brien na Jeffrey Feltman wameonya dhidi ya tatizo la ukosefu wa fedha kwaajili ya kusaidia mapambano dhidi ya kundi hilo.

Kundi la Boko Haram limeendelea kuzilenga nchi za Nigeria na Cameroon kwa kutumia mabomu na mauaji ya kujitoa mhanga.

Wiki iliyopita shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) lilionya kuwa karibu watoto 250,000 kwenye baadhi ya maeneo ya nchi ya Nigeria ambayo yalikuwa yakikaliwa na Boko Haram wanakabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo.

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 likiwa na lengo la kuipinga elimu ya kimagharibi kabla ya kuanza harakati za kijeshi mwaka 2009.

LEAVE A REPLY