UN yaionya Sudan Kusini

0
78

Umoja wa mataifa umemuonya rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir kwamba utaratibu wa kuwaajiri au kuwafuta kazi maafisa wa ngazi ya juu serikalini lazima ufuate masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini miaka miwili iliyopita.

Mkataba huo ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka baada ya rais huyo kumfuta kazi makamu wake wa rais na mpinzani wake Riek Machar.

Machar aliondoka Juba mapema mwezi huu baada ya mapigano makali kuzuka baina ya wanajeshi wanomuunga mkono na wale wanaomuunga mkono rais Kiir,ambapo silaha nzito nzito zilitumika kama vile vifaru na helikopta za kijeshi.

Mkataba wa amani wa Agosti unaweka wazi kwamba makamu wa rais sharti achaguliwe na kambi ya upinzani.

Machar alichaguliwa tena na kupishwa tena kama mwenyekiti wa kwanza hapo mwezi Aprili.

Lakini Machar alipoondoka Juba kutokana na mapigano yaliyozuka nje ya kasri ya ,rais, Kiir akamchagua Brigadia Taban Deng ambae ni waziri wa madini nchini humo kuchukua nafasi ya Machar.

Inasemekana uchaguzi wa Brigadia Taban Deng uliafikiwa baada ya kikao cha wapinzani wa Machar katika kundi lao la Sudan People’s Liberation Movement in-Opposition (SPLM-IO) ambao vinara wao wanapingwa na wafuasi wa Machar.

LEAVE A REPLY