Umri wa miss Tanzania 2016 ‘walindwa’. Elimu je?

0
531

Mlimbwende mpya wa Tanzania ambaye alipatikana usiku wa kuamkia Jumapili jijini Mwanza, huenda akalazimika kufanya mazoezi ya kuwahimili waandishi wa habari na kujibu meseji za watu kwenye mitandao ya kijamii bila kuchanganya maneno.

Hayo yamekuja kufuatia malalmiko ya wadau wa shindano hilo kudai kuwa kwa mara nyingine tena Tanzania imepata mlimbwende ‘anayepitiliza vigezo’ ikiwemo umri.

Hali hiyo iliyozua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii ilijibiwa na kambi ya mlimbwende huyo kama ifuatavyo:

Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

  1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni. 
  1. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.
  1. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.
  1. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya “Character assassination” lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

 Hiyo ilikuwa taarifa iliyotolewa na kaimu afisa habari wa mlimbwende huyo Charles William.

Kigezo cha umri huenda kimefanikiwa kulindwa kwa maslahi ya mlimbwende, vipi kuhusu elimu na huko aendako?

LEAVE A REPLY