Umoja wa Mataifa wapiga kura kupunguza waangalizi wa amani DR Congo

0
118

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya kupunguza ukubwa wa jeshi lake Monusco, ambalo ndio jeshi kubwa zaidi na ghali zaidi ambalo liko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika mkakati mpya ambao unaendela kufanyiwa kazi, wanajeshi hao wa kulinda amani watapunguzwa kutoka 19,000 hadi 3,000.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuvunjika kwa makubaliano ya kisiasa yaliyoingiwa kati ya kanisa Katoliki na Serikali ya nchi hiyo yaliyositisha maandamano ili kuruhusu uchaguzi wa raisi, hali inayopelekea nchi kuwa katika hatari ya machafuko.

Baadhi ya mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa wameonyesha dalili za nia ya kupunguza misaada kwaajili ya ulinzi wa amani hususani utawala mpya wa Marekani chini ya rais Donald Trump ambao ndio mchangiaji mkubwa.

Siku ya Jumatano, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Hailey, alidai Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali ‘dhalimu’ nchini Congo na akataka jeshi la Monusco lipunguzwe.

Monusco lilikuwa jeshi muhimu kwenye kuwadondosha waasi wa M23, kundi kubwa la waasi nchini DR Congo. Hata hivyo Monusco limekuwa likikabiliana na maandamano ya vurugu na mashambulizi kutoka kwa raia ambao wanalituhumu jeshi hilo kwa kutofanya kazi yake sawa sawa.

LEAVE A REPLY