Umoja wa Afrika (AU) kumpata Mwenyekiti mpya leo

0
229
AU: Nembo ya Umoja wa Afrika

 

Marais na viongozi mbalimbali wa kitaifa ambao wanawawakilisha marais wa nchi zao wako jijini Kigali nchini Rwanda wakipiga kura ya kumchagua mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU) ambaye atachukua nafasi inayoachwa wazi na Nkosazana Dlamini-Zuma.

Bi. Zuma ameamua kuachia wadhifa huo baada ya kuutumikia kwa muhula mmoja wa miaka minne.

Wagombea wa nafasi hiyo kwa sasa ni:

  • Makamu wa zamani wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe
  • Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Botswana Pelonomi Venson-Moitoi
  • Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Equatorial Guinea  Agapito Mba Moku

Wakati huo huo mfalme Mohammed VI wa Moroko ametuma ujumbe kwenye mkutano huo wa Rwanda kuomba nchi yake kurejea kwenye umoja huo baada ya kukaa nje kwa miaka 32.

Moroko ilijitenga na AU mwaka 1984 baada ya Umoja huo kuutambua uhuru wa Sahara Magharibi nchi ambayo Moroko inadai ni sehemu yake.

AfricanUnion-flag

LEAVE A REPLY