Ukweli kuhusu baba mzazi wa msanii Diamond Platnumz

0
52

Aliyekuwa baba wa Diamond Platnumz, Mzee Nasib Abdul amesema alitoa kauli ya kuwa Diamond asitumie jina lake lakini kwa sasa hana shida ikiwa msanii huyo ataendelea kutumia jina lake.

Mama wa mzazi wa msanii wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim maarufu kwa jina la mama Dangote kusema kuwa aliyekuwa anafamika kuwa ni baba mzazi wa msanii huyo si baba mzazi bali ni baba mlezi.

Kwa muda mrefu ilikuwa ikifahamika na wengi kwamba baba mzazi wa Diamond ni mzee Abdul Juma Issack na ndio maana msanii huyo alikuwa akitumia jina halisi la Naseeb Abdul Jumaa.

Jambo hilo lilisabababisha baba Diamond naye kulizungumzia na kufika hatua ya kutaka msanii huyo kuanzia sasa asitumie jina la Abdul na kuahidi kama ataendelea kulitumia atamshtaki.

Pamoja na hayo, alisema kiekweli kitendo alichokifnaya mama Diamond kama binadamu hajakifurahia kwani amemvua nguo mbele za watu na kueleza kwamba ameamua kumuachia Mungu ndiye muamuzi wa yote.

Hata hivyo alipoulizwa kama haiwezi kumuathiri msanii huyo katika shughuli zake za kibiashara, alisema hakuna kitu kama hicho kwani jina la kibiashara analolitumia ni Diamond Platnumz na sio Naseeb Abdul.

Mama Diamond alieleza sababu ya kumpa jina la Naseeeb Abdul badala ya Naseeb Salim Nyange baba ambaye mama Diamond anaeleza kuwa ndio mzazi, mama huyo alisema ni kutokana na siku aliyokwenda kujifungua mzee Abdul ndiye aliyempeleka hospitali.

LEAVE A REPLY