Ukaribu wa Baba Levo na Shilole

0
23

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amefunguka ukaribu wake na msanii Shilole ambao umedumu kwa muda wa miaka 12 hadi sasa toka wajuane.

Baba Levo amesema Shilole alikuwa mwanamke mzuri na aliamini akiwa naye karibu atavutia japo wakati wanaanza urafiki wao alimpenda ukweli kutoka moyoni.

“Mimi na  Shilole tuna miaka zaidi ya 12 au 13, alikuwa mwanamke mzuri halafu nilikuwa sina pesa ila niliamini nikiwa naye karibu nitanukia.

Mwanzo nilikuwa nampenda kutoka moyoni, na mahusiano yake mengi mimi ndiyo nimemkonektia kwa wanaume kuanzia Nuh Mziwanda, Nedy Music na wengineo, pia nilikuwa nampa ushauri”.

“Shilole anapenda sana na akishapenda sehemu yeye ni wivu tu, ugomvi, mkorofi na anapenda sana kutawala, kwa hiyo unajikuta unaanza kuamua kesi baada ya kesi, kwa mfano kesi za Nuh na Shilole nimeshaziamua zaidi ya mara 56”.

LEAVE A REPLY