Ukame waitesa Zimbabwe

0
301

Shirika la kimataifa la kusaidia watoto la ‘Save the Children’ limetoa onyo kuwa huenda maelfu ya watoto nchini Zimbabwe wakakabiliwa na njaa kali au vifo vitokanavyo na ukosefu wa chakula kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Utafiti wa shirika hilo umeshagundua kuwa watoto 200 tayari wameshafariki kutokana na ukosefu wa chakula katika kipindi cha mwaka nmmona na nusu uliopita.

Ukosefu huo mkubwa wa chakula unatokana na ukame mkubwa ulioikumba nchi hiyo.

Mmoja wa maafisa wa shirika hilo, Tanya Steela amedai kuwa baadhi ya kina mama hukaa hadi siku tano bila chakula na wahudumu wa afya huwapa watoto wao matunda mwitu kabla ya kugundua watoto wana dalili za utapiamlo.

Takwimu za wizara ya afya ya Zimbabwe zinbaonyesha kuwa watoto 946 wanakabiliwa na utapiamlo mkali na idadi ya watoto hao inatarajiwa kuongezeka kwa kasi kwenye miezi michache ijayo.

Takwimu za vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwenye mji wa Binga zimeripotiwa kuongezeka mara tatu zaidi ambapo kwa sasa vimefikia vifo 200 katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita.

Zimbabwe ni moja ya nchi za kusini mwa Afrika zilizokumbwa na ukame mkubwa na maafisa wa serikali wanakadiria zaidi ya watu milioni 4 watakumbwa na njaa kufikia mwisho mwa mwaka huu.

LEAVE A REPLY