Ujumbe wa Tommy Flavour kwa Alikiba

0
31

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour ameandika ujumbe mzito sana akiushukuru Uongozi wa Kings Music kumsimamia katika muziki na kumfanya leo ajulikane Tanzania nzima.

“Nakumbuka hapo nyuma kidogo kipindi cha miaka kama kumi na tano au sita kipindi bado niko shule nakumbuka kipindi hicho ndio Cinderella ya Alikiba imetoka.

For sure kwa wakati huo sikuwa hata kama nafaham nina uwezo wa kuimba ila nilikua napenda sana kukariri nyimbo tofauti toka kwenye radio magazeti na tv tu so hata baadhi ya wasanii walikua hatuwafaham kwa sura ila kazi Zao bado zilikua zinafanya vizuri.

Basi kwa wakati huo nilikua shabiki wa MB dog sana ,siku moja niliusikia wimbo wa Cinderella radio kwa kweli ulikua ni wimbo wa pekee ambao sikuwa nimewahi sikia msanii mwingine kuimba hivyo japo nilikua napenda sana hihop music ila kwa upande mwingine nikaamini mwenye huo wimbo atakua MBdog tu..basi nilikutana na brother mtaani yeye alikua nae anafanya music hapo kitaa nikamuuliza.

Kaka kuna wimbo mpya nimeusikia mara moja kwenye radio ni mkali sana wa nani huu itakua mbdog maana kuna baadhi ya watu tuliamini hivyo ..jamaa akaniambia embu Imba kidogo niusikie.

Basi nikajaribu kuuimba mbele yake hakuamini kama ningeweza kua na sauti ya kumvutia na nikauimba ule wimbo vizuri kwa jinsi alivyokua ananijua ni dogo tu wa kitaa, akaniambia unajua dogo unasauti sana.

Una uwezo wa kuimba ujue…unaweza ukafanya music una kipaji mbona…huyu ndio alikuwa ni mtu wa kwanza kugundua nina uwezo mpaka leo hii hapa nilipofika.

Miaka 15 baadae naishi kwenye ndoto zangu, namshukuru Manager wangu kwa kuniwezesha kutimiza ndoto zangu – nakushukuru Alikiba kwa kuniingiza rasmi kwenye dunia ya muziki – Allah akuzidishie pale ulipopunguza kwa ajili yangu mimi na wasanii wengine ambao umewahi kuwasaidia.

Wimbo wangu wa kwanza chini yako Omukwano umefikisha views millioni, tena kwenye account yangu binafsi ambayo ilikuwa mpya, kwa wengine huenda ikawa jambo la kawaida ila kwangu ni mafanikio.

LEAVE A REPLY