Ujumbe wa Roma kwa mkewe baada ya kutimiza miaka mitano ya ndoa

0
25

Mwanamuziki wa Hip Hop, Roma Mkatoliki ametimiza miaka mitano ya ndoa yake na mkewe ambapo wamesheherekea kwa kutumiana ujumbe wa kupongezana na kutakiana kheri kwa walipo na wanapoelekea.

Kupitia ukurasa wa Instagram anaoutumia Roma Mkatoliki, ametoa historia fupi kuhusu mahusiano yao yalipoanzia ambapo ameeleza.

Ameanza kwa kusema kuwa “Nakumbuka kipindi kile miaka zaidi ya 11 iliyopita, ulivyokuwa unanitongoza nakukatalia, ukanitongoza mara ya pili nikakuchomolea ukawa unalia sanaa daaaah, mara ya tatu nikaja kukuonea huruma nikakukubalia tukaanza mahusiano, leo tuna miaka mitano kwenye ndoa yetu hakika Yehova ni mwaminifu”

Ameongeza kwa kusema kuwa “Huku kila nikitaka kuku-cheat inanijia ile sura yako ukilia mbele ya waandishi wa habari kipindi nimetekwa, ikinijia tu basi hisia zote zinakata naishiwa nguvu nawafukuzia mbali wazungu, navuta shuka nalala peke yangu, Mungu aendelee kudumisha ndoa yetu usiache kuniombea Shetani asije akanihadaa nami nafanya hivyo pia”.

Kwenye ndoa wamebarikiwa kupata watoto wawili ambao ni Ivan na Ivy, na kwa sasa msanii huyo wa HipHop yupo nchini Marekani tangu alivyoondoka Tanzania mwishoni mwa mwaka 2019.

LEAVE A REPLY