Ujumbe wa Mwana FA kwa mashabiki zake

0
131

Msanii wa Hip Hop Bongo, Mwana FA amewataka mashabiki wake kuacha tabia ya kutangaza matangazo yao kwenye posti zake anazowekwa katika akaunti yake ya Instagram.

Mwana FA amewachana mashabiki wake hao kuwa wanamkwaza kwa kuandika ‘comment’ za matangazo kwenye ‘post’ zake anazoweka kwenye mtandao wa Instagram.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa umetoka rohoni mwake, huku akiambatanisha picha mpya ambazo zinaonesha sio mazingira ya kawaida na kudhaniwa ni ‘Location’ ya ‘video’ yake mpya.

Baada ya kuandika hayo mashabiki wake wamemcharukia staa huyo kwa kumwambia waondio wamemuongezea idadi ya wafuasi mitandaoni, hivyo anavyowazuia kutangaza biashara zao nao wanaweza kuamua kutomfuata na mwisho wa siku hatakuwa na wafuasi.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa na tabia ya kuweka matangazo yao ya kibiasha kwenye posti za watu maarufu ambapo baadhi ya watu hao maarufu wameonekana kukelwa na tabia hiyo.

LEAVE A REPLY