Ujumbe wa Monalisa

0
17

Mwigizaji wa filamu nchini, Monalisa amewataka wananwake ambao wako kwenye ndoa waache kujisheua na badala yake wajiulize kama wanaume zao hawana watoto wa nje.

Kauli hiyo ameitoa kupitia akaunti ya mtandao wake wa Instagram, baada ya kudai kuwa amekuwa akiulizwa maswali mengi, ambayo watu wamekuwa wakionesha kushangazwa na yeye kuwa na watoto ambao kila mtoto na baba yake.

“Sioni haya hata kidogo tena ‘am so proud’ kuwa mama wa watoto hawa na kutangaza hadharani kwamba kila mtoto ana baba yake, na baba zao wanajijua na ni baba zao hasa”, ameandika Monalisa.

Aidha Monalisa akaongeza kuwa, “Ujumbe kwako ni huu, wewe unayejiona ni Malaika kwamba upo kwenye ndoa na una watoto halali jitathmini kabla hujaninyooshea kidole, kama ni mwanaume angalia vizuri wanao, kweli ni wako? kama ni mwanamke usijishaue, jiulize mumeo hana mtoto nje?”.

LEAVE A REPLY