Ujumbe wa Ibrah kwa Harmonize

0
41

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrah amemuandikia ujumbe wa kumshukuru boss wake Harmonize ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo kwa upendo wake.

Ibrah amemshukuru Harmonize kwa kutambua kipaji chake na kusema kuwa bila yeye asingekuwa na uwezo wa kutunza familia yake na Sasa yeye ndio tegemeo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ibraah ameandika “Bila Wewe Siku Kama Ya Leo Ningekuwa Zangu Naimba Imba Mtaani Ili Nipate Pesa Angalau Ya Mama Kununua Chakula Ale na Wadogo Zangu.

Lakini Leo Nimekuwa Tegemeo Kwa Familia Japokuwa Umri Wangu Mdogo! Yote Haya Ni Sababu Ya Wewe,Nakushukuru Sana Na Milele Utakuwa Kwenye Moyo Wangu,Wewe Ni Baba Na Nakutegemea Sana Wewe Kufikia Malengo Yangu.

Nilipoteza Matumaini,Sikujua Kama Kuna Siku East Africa Itanijua Na Kunipenda,Haya Yote Wewe Ndio Sababu! Nakuombea Mungu Azidi Kukuinua Na Aendelee Kukupa Moyo Wakusaidia Na Wengine.

LEAVE A REPLY