Ujumbe wa Harmonize kwa Rayvanny

0
173

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amemlaumu msanii mwenzake Rayvanny kwa kuvujisha video zake za kimahaba na mtoto wa msanii mwenzake, Kajala Masanja aitwaye Paula.

Harmonize amesema kuwa kitendo alichokifanya msanii mwenzake huyo hakiaksi usanii na badala yake kimemshushia heshima huku akimtahadharisha kuwa anayo kesi ya kujibu na iwapo Serikali itaamua kulifuatilia sakata hilo.

Kupitia akaunti yake Instagram Harmonize ameandika ”(Ray) you are my young brother and yafuatayo sitoyasema kama mimi ni mzazi wa Paula no, naandika kama mzazi niliye na mtoto wa kike (Zurekha) lakini pia kama msani mwenzako (Ray ) najiuliza tuu..!!

Ulipata wapi ujasiri huu wa kutembea na mwanafunzi wa kidato cha (5) wakati ni wazi ya kwamba ni kosa la jinai, hukumu yake sio chini ya miaka 30 lakini pia isitoshe una record na video ukiwa una kiss yaani unaonyesha kwamba serikali haiwezi kukufanya kitu, nawaza lengo lilikuwa ni kuonyesha kwamba upo juu ya sheria?

Hebu angalia future ya mtoto wa watu umeiweka wapi kwa tamaa za siku 1 kama kweli mlikuwa mnapendana mko in love video ilikuwa na haja gani and lengo la kuvujisha nini?

Lakini pia serikali itajiuliza una videos ngapi za watoto wa shule kama umeweza kuwa na hii na ukaivujisha? Je, uliwaza wasichana wa rika lake ambao walikuwa mashabiki zako watafurahishwa na hichi kitendo cha kinyama? Maana kama leo umemfanyia mwenzako ni wazi kesho utawafanyia wao.

Huoni kama umewapoteza mashabiki imara! Wataipata wapi nguvu ya kujirecord ngoma zako na kupost ikiwa umemdhalilisha msichana mwenzao mdogo (kingono )? Je, kuhusu wazazi wenye watoto wa kike watakutazama sura gani?

Usisahau kuna vijana wenzio ambao wana wadogo zao wa kike watakuonaje? Kwa nini usiendelee kuimba muziki tu huhitaji kujiingiza katika kuhatarisha maisha yako kama hivi, tazama mifano ya wasani wakubwa akina R Kelly mpaka leo wanasota ndani kwa ajili ya mambo hizi za watoto wa (shule).

Kama tatizo lilikuwa ni mimi kumpenda mama yake (P) na watu wengi wakavutiwa na sisi si ungetafuta mkubwa mwenzio why (mwanafunzi) tena wa miaka hii ya (JPM), serikali ya leo ipo macho sanaaa. Maana watendaji wengi ni vijana. Je, watakubaliana na hili unadhani waziri wa sanaa michezo na burudani atakalia kimya?

Umejiuliza mashirika yanayosimamia haki za wanawake watalifumbia macho? Mamlaka za elimu je? Richa ya yote you’re still my brother, ila trust me hili suala limeniumiza kama kijana niliyebarikiwa mtoto.

LEAVE A REPLY