Ujumbe wa Diamond kwa mpenzi wake Tanasha siku ya Valentine

0
245

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameisherehekea na kuimaliza Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) vizuri  kwa kutuma zawadi na kuandika ujumbe wa mahaba kwa mpenzi wake Tanasha Don.

Diamond ameweka picha katika akaunti yake ya Instagram iliyoambatana na ujumbe unaosomeka, “Kwasababu wewe ni mpendwa wangu milele.

Pia ameendelea kuandika “ Natumaini utapenda zawadi yangu ndogo ya kushangaza…japo upo mbali lakini moyo wangu upo nawe kwaajili yako”.

Kwa upande wa mpenzi wake huyo toka Kenya Tanasha Don pia alishukuru zawadi aliyotumiwa na mpenzi wake huyo ambayo ilikuwa kwenye picha yenye maneno, ‘I love You Tanasha’ huku yakiwemo maua na box za zawadi.

Tanasha nae akajibu “Asante mpenzi wangu, mimi ni mwanamke wa bahati sana kuwa na wewe katika hii dunia.  Maneno hayawezi kuonyesha jinsi gani ninavyojisikia kwa wakati huu”.

LEAVE A REPLY