Ujumbe wa Billnass kwa Nandy

0
37

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amemuandikia ujumbe mpenzi wake Nandy kwenye siku yake kuzaliwa iliyofanyika hapo jana.

Billnass ameandika ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram unaosomeka kama ifuatavyo kwenye mtandao huo.

“Leo, nataka ujue jinsi ulivyo Muhimu kwangu, Kwanza Sikuwahi Kujuwa kuwa Ulimwengu wa Mapenzi ni Mtamu Hivi, Wewe ni Mwanamke wa kipekee Sana.

Napenda Ulivyo na Uelewa, Napenda Ulivyo Msikivu unajuwa Kujali, Una Subra, Una fadhila na mkarimu, Nahisi Kama Nimependelewa Sana Kuwa Na Mwanamke Mzuri Sana na Mwenye Kila Ninalohitaji… Nakupenda Sana, Na Kila iitwapo Leo Nazidi Kukupenda zaidi.

Heri ya mfanano na siku yako ya kuzaliwa mke wangu mtarajiwa rafiki na kipenzi cha mama yangu. Mwenyezimungu akupe hitaji la moyo wako.

Huu ni ujumbe wa kwanza wa kumtakia kheri kwenye kumbukizi ya kuzaliwa mrembo huyo tangu waweke wazi mahusiano yao ya kimapenzi kwa kuveshana pete mwezi April ,19 mwaka huu.

LEAVE A REPLY