Uingereza kujitoa EU mwakani

0
139

Serikali ya Uingereza imetangaza msimamo wake kuwa hatua ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya haiwezi kuanza kutekelezwa kabla ya kuisha kwa mwaka huu.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande aliyetarajiwa kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May jioni ya jana alisema kuwa anatarajia kumwambia Bi. May aharakishe mazungumzo ya kukamilisha mchakato wa Uingereza kujitoa EU na pasiwepo na makubaliano ya awali.

Msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya rais Hollande alisema: ‘Msimamo wa waziri mkuu uko wazi na hayo ndiyo maamuzi ya serikali ya Uingereza ya kuamua muda wa kufanya iutekelezaji wa kifungu cha 50’

Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya mapema mwezi Juni mwaka huu ingawa bado kumekuwa na mitazamo inayokinzana juu ya mustakabali wa taifa hilo iwapo azma hiyo itatekelezwa.

Nchi za Scotland na Ireland ya Kaskazini ambazo ni sehemu ya Uingereza zimeshaeleza msimamo wake wa kuipinga hatua hiyo ya kujitoa na zinatafuta namna ya kubaki kwenye Umoja huo.

LEAVE A REPLY