UGAIDI TENA UFARANSA 84 WAUAWA

0
248

Watu 84 wengi wao wakiwa watoto wadogo wameuawa kwenye shambulio jengine la kigaidi nchini Ufaransa huku watu wengine 18 wakiwa katika hali mbaya sana.

Mshambuliaji ametumia lori kuwagonga watu waliokuwa wakiadhimisha sherehe za siku ya Bastile kusini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Nice.

Polisi wamefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi muuaji huyo.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amesema kuwa nchi yake iko kwenye vitisho vya ugaidi wa makundi yanayojinasibisha na imani ya dini ya kiislam.

Tayari Ujerumani na viongozi wa mataifa mengine ya Ulaya na viongozi wa taasisi za kimataifa wametangaza kusimama kidete na Ufaransa ili kushirikiana kwenye vita dhidi ya ugaidi.

Hili ni tukio jengine kuikumba Ufaransa kwenye siku za karibuni ambapo miezi michache iliyopita mashambulizi ya kigaidi yalitokea kwenye uwanja wa mpira pamoja na klabu ya usiku.

 

UFARANSA

Ugaidi: Picha ya lori lililotumiwa na gaudy kuua watu 84 Usiku wa kuamkia leo likiwa na mutant ya risasi. 

LEAVE A REPLY