Uchebe akataa kuongelea ndoa yake

0
27

Aliyekuwa mume wa msanii Shilole aitwae Uchebe amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kuongelea tukio lililopita kwa kumesema hawezi kumpa mtu faida kwa sababu yeye ndiyo alikuwa kwenye ndoa.

Uchebe amefunguka hilo baada ya kutukanwa na kushambuliwa mitandaoni kuhusu kusambaa kwa picha ambazo zilionyesha amempiga mke wake Shilole ambapo mwenyewe ameeleza kuwa,

“Naweza nikasema kwamba siwezi nikampa mtu faida ya kidunia kwa sababu hata nikimuomba pepo hawezi kunipa.

Pia amesema kuwa vitu vingine mimi kama mwanaume ambaye nilikuwa kwenye mahusiano ya ndoa iliyohalalishwa na Mungu siwezi nikamfaidisha mtu wa nje ila ikifika wakati nitazungumza ila kwa sasa hivi sina lolote la kusema, hakuna kitu kibaya kama mambo ya siri ukayaweka bayana” ameeleza Uchebe.

Wiki iliyopita Shilole alipost picha kwenye mtandao wa Instagram zikimuonyesha ana damu na alama usoni mwake na kueleza kwamba huwa anapigwa na Uchebe.

LEAVE A REPLY