Uchebe afunguka madai ya kumpiga Shilole

0
90

Baada ya kusambaa kwa picha za mwanamuziki Shilole kupigwa na Mume wake Uchebe, mwanaume amefungukia madai hayo ya kumpiga mke wake huyo.

Taarifa hizo zilisema kwamba Shilole amekuwa akishushiwa vipigo na mumewe huyo, hivyo kuamua kuwa muwazi kwa jamii na hata kutangaza kuikataa ndoa yake.

Uchebe amesema picha hizo zilizowekwa Instagram na mkewe Shilole hazina uhalisia wa kipindi hiki kwani ni za muda mrefu kabla hata hawajafunga ndoa.

Pia amesema kuwa “Wanawake Wasanii mtihani sana, Allah awafanyie wepesi. Hizo za enzi hizo, kipindi hicho Shilole hajaacha mambo yake. Kitambo sana, muda mrefu sana hata kumuoa sijamuoa.”

Pia suala la Shishi kusema kwamba Ndoa yao imevunjika, Uchebe amesema anamuachia Mwenyezi Mungu kutokana na kitendo hicho cha mwanamuziki huyo.

LEAVE A REPLY