Ubonge wamsumbua Aika

0
92

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuweka wazi Jinsi miwili mkubwa unavyokuwa unamnyima raha hasa stejini.

Aikah ambaye ameonekana kukosolewa sana na mashabiki zake hasa katika Mitandao ya kijamii amefunguka na kukiri kuwa anajua kabisa ameongezeka sana lakini anafanya jitihada za kupungua.

Aika alisema amekuwa akiteseka na ubonge alionao kwa sasa kwani haupendi na watu mbalimbali wamekuwa wakimshangaa na kumtaka aanze kufanya mazoezi kwani anapoteza mvuto.

Aikah ambaye ana Mtoto wa mwaka mmoja na Mpenzi Wake Nahreel ameweka wazi kuwa alizidi kuongezekabzaidi Baada ya kujifungua mwaka jana.

 

LEAVE A REPLY