Tyrese aachana na mkewe

0
9

Mwimbaji na Muigizaji wa Marekani, Tyrese Gibson ametangaza maamuzi magumu ya yeye na mkewe Samantha Lee Gibson kufikia uamuzi wa kupeana talaka.

Tyrese ametoa tamko hilo jana Jumanne kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika wametalikiana na mkewe Samantha lakini lengo lao ni kubaki marafiki na wazazi wanaoshirikiana vyema.

Wawili hao walifunga ndoa February 2017 na kubarikiwa kupata mtoto mmoja wa Kike, Soraya mwaka 2018.

Hii ni ndoa ya pili kwa Tyrese kuvunjika kwa talaka, mwaka 2009 alitalikiana na Norma Mitchell ambaye walifunga ndoa mwaka 2007 na kupata mtoto mmoja wa Kike, Shayla.

 

 

 

LEAVE A REPLY